Na Magreth Mbinga
Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Amani duniani Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es salaam inayoongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo imetoa tamko ambapo imeitaka jamii kuendelea kuilinda na kudumisha amani ili kuwa Taifa lenye maendeleo kwani hakuna maendeleo bila ya kuwa na Amani na utulivu.
Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Habari wa Kamati hiyo Catherine Lukindo amesema kuwa uwepo wa Vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo matukio ya uhalifu yanayofanya na kundi la Panya Road hurudisha nyuma maendeleo kwani kujenga hofu miongoni mwa jamii.
Aidha Afisa habari huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Wazazi kufuatilia mienendo na malezi ya watoto wao ili kuwaepusha vijana wao kujiunga na vikundi vya kihalifu.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo Athuman Mlimasunzi ametoa rai kwa Watanzania wote kuwaunga Mkono viongozi wa Kitaifa na viongozi wa dini katika kudumisha amani.