Home Kitaifa MATAWI 197 YA UMOJA WA WAZAZI CCM YAPATA KADI NA MIHULI

MATAWI 197 YA UMOJA WA WAZAZI CCM YAPATA KADI NA MIHULI

Jumla ya matawi ya Jumuiya ya wWazazi CCM 197 wilayani Sengerema mkoani Mwanza yameondokana na ukosefu wa mihuli na kadi za jumuiya hiyo baada ya Mwenyekiti wa wilaya Ndugu Jacksoni Mazinzi kuchonga mihuli na kununua kadi zaidi ya 2000 na kuigawa bure kwa kila tawi kwa lengo la kuondoa changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na viongozi waliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake na kamati utekelezaji amesema mihuli na kadi za jumuiya ni sehemu ya ahadi yake kwa wajumbe ambapo walimtaka akishika kijiti cha uongozi awatatulie changamoto hizo “wakati nagombea mlinitaka nitatua changamoto za kadi na mihuli na mimi nimefanya hivyo mnakumbuka niliahidi kadi elfu moja lakini kulingana uhitaji nitatoa kadi bure 2250 kwa kata zote 47 za wilaya ya Sengerema niliahiadi natekeleza”

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Sengerema Jamali Athuman alitumia ziara hiyo kuwakumbusha wajumbe na wananchama wa jumuiya hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi waliopo madarakani na kuendelea kusemea mazuri yanayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluu Hassan hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika wilaya hiyo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi kamati ya Utekelezaji waliongozana na mwenyeki Dickson Mtaka na Josephat Makoli…walishauri kuwa ziara hiyo isiishie katika jumuiya ya wazazi badala yake kila jumuiya iwafikie wanachama viongozi ili kuwasikiliza na kutatua kero zao kuliko kusubili wakati wa uchaguzi.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!