Home Kitaifa Masomo ya Sayansi toka Shule za awali ni Muhimu

Masomo ya Sayansi toka Shule za awali ni Muhimu

Na Neema Kandoro, Mwanza

MASOMO ya sayansi yanapaswa kuanza kufundishwa tangu shule za awali ili kujenga misingi mizuri ya wanafunzi kukua wakipenda kujifunza mtaala huo ili kuwezesha taifa kupata wanafunzi wengi watakaosomea fani hiyo.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Mwanza na wadau mbalimbali wa elimu kwenye shule ya Awali na Msingi Splendid Stars wakisema kitu ambacho nchi inataka wanafunzi watilie maanani inapashwa kuandaliwa mapema katika umri mdogo.

Mkazi wa Kisesa wilayani Magu Claudian Mwita ambaye mwanaye Moses Mwita ameanza shule ya awali hapo na sasa ataanza mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi alisema mtoto huyo anataka kusoma zaidi masomo ya sayansi kwenye shule ya sekondari.

“Wazazi kutokana na shughuli za kimaisha zinazosababisha kutokukaa na watoto wetu wadogo siku nzima upo umuhimu wa shule za awali ziwezeshe watoto wapende masomo ya sayansi” alisema Mwita.

Alisema kutokana na wanafunzi kufundishwa wakiwa wadogo masomo ya sayansi kinadharia na kwa matendo imemujenga kimawazo na kisaikolojia mwanaye kutaka kuendelea kusoma masomo hayo zaidi.

Meneja wa shule hiyo Jane Malegesi alisema kuwa kwa kutumia vitu ambavyo siyo vya gharama kubwa wanawafundisha wanafunzi hao masomo ya sayansi kwa nadharia na kwa vitendo hivyo huwaongezea watoto ari ya kutaka kujifunza zaidi.

Alisema tunataka watoto waendane na dunia ya leo ambapo matumizi ya analojia yanaondoshwa na matumizi ya dijitali kwa sasa hivyo upo umuhimu wa mitaala yetu kujibu mahitaji ya taifa kwa sasa.

Dunia yetu ya sasa tunalazimika kuweka juhudi za kuwaandaa watoto wetu kwa masomo hayo kwani matumizi ya Teknolojia yana nafasi kwenye kila nyanja kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!