Home Kitaifa MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOFANYA KAZI MARA YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOFANYA KAZI MARA YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

Na Shomari Binda-Musoma

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali ( NGO’s) yanayofanya kazi mkoani Mara yametakiwa kuzingatia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya nchi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi alipokuwa akizungumza na mashirika hayo leo januari 29 kwenye ukumbi wa uwekezaji uliopo kwenye ofisi hizo.

Amesema mashirika yanayofanya kazi Mara yanafanya kazi nzuri kwa kushirikiana na serikali lakini yapaswa kukumbushana kuzingatia Sheria za nchi.

Mtambi amesema anatambua mkoa wake una jumla ya mashirika 200 ambayo yamehakikiwa na msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali na kwa sasa ndiyo yanayotambulika japokuwa mkoa unaendelea kupokea maombi ya usajili kwa wadau.

“Lengo la Mkutano huu ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu uratibu na usimamizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na kujadili mchango wao katika maendeleo ya Mkoa

“Kubainisha namna shughuli za mashirika zinavyoweza kwenda sambamba na miongozo ya kitaifa pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali hivyo ni kikao muhimu”,amesema

Amesema anatambua amekutana na viongozi wa Baraza la “NACONGO”Taifa, Mwenyekiti wa NGOs Mkoa wa Mara, Msajili Msaidizi wa NGO’s Mkoa, Wasajili wasaidizi wa NGO’s wa Halmashauri, Wadau wote wa Mashirika yasiyo ya kiserikali na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara na kutaka kuzingatia ujumbe wake.

“Napenda kuwashukuru kwa namna ambayo mnashirikiana na mkoa katika kufanya kazi za kuleta maendeleo kwa jamii yetu na kutoa elimu na huduma mbalimbali na kujenga miundombinu na imepelekea kuacha alama kutokana na kazi mnazofanya hongereni sana.

Akizungumza katika mkutano huo Hajat Mwantumu Mahiza ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ameishukuru serikali mkoa wa Mara kwa kuwapokea na kuwapa ushirikiano.

Amesema lengo la mkutano na kikao hicho ni kuyakumbusha mashirika kuzingatia ulipaji ada na kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali.

“Nipo mkoani Mara baada ya kuchagua sampuli ya mikoa michache ili kupunguza mashirika yaliyosajiliwa kufutwa lakini kuamasisha ulipaji wa ada ya mashirika haya na hapa Mara ni mkoa wa nne kati ya 26″,amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!