Home Kitaifa MASHIRIKA YANAYOJIHUSISHA NA KUTOA MISAADA KWA WATU WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI YAPONGEZWA

MASHIRIKA YANAYOJIHUSISHA NA KUTOA MISAADA KWA WATU WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI YAPONGEZWA

Na Magrethy Katengu– Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa pongeze kwa Mashirika yote yanayojihusisha na kufanya matendo ya huruma kuokoa maisha ya watu walio katika mazingira hatarishi kama kwenye vita, mafuriko, majanga ya moto, kwa kutoa misaada ya kiutu bila kujali maisha yao.

Pongezi hiyo ameitoa Agosti 14, 2024 katika Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya watoa kwa binadamu Agost14–18 mwaka huu iliyoongozwa na kauli mbiu isemayo ” tenda kibinadamu” ambapo amesema watu hao wamekuwa wanafanya kazi kubwa sana hatarishi kwani wengine wamepoteza maisha wakipeleka vyakula nchi zilizokubwa na vita .

” Siku hii ni ya tafakari sana kwani tunaona haya mashirika Tanzania ilipopata madhara ya hapa na pale walijitokeza kutoa misaada mfano maporomoko ya Hanang’i ambapo baadhi ya watu walipoteza maisha wengine kupoteza makazi na raslimali hawa walikwenda huko kila mmoja kutoa misaada ya kibinadamu ya vyakula, nguo na hata kuwasaidia wanafunzi baadhi ya mahitaji waende shule” Mpogolo

Hata hivyo Mkuu wa Mkuu wa Wilaya amesema Mungu alimuumba mwaadamu hivyo hata kutenda matendo ya uanadamu unaambatana na matenda na roho ya upendo aliyojaliwa na Mungu

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kutoa msaada ya Kibinadamu (DINGONET –DISASTER NGO’S NETWORK) Ruger Kahwa amesema wanaofanya shughuli hizo za kuokoa maisha ya wanadamu walio katika umoja huo wako 18 na wamekuwa wakenda maeneo hatarishi kutoa msaada na baadhi yao walipoteza maisha wakiwa katika utekelezaji wa kusaidia kuokoa roho za watu akitolea mfano vita vya Irac kuna mashujaa wao walipoteza maisha kwa kulipuliwa na bomu wakiwa wanawapa chakula waathirika wa vita hivyo kazi hiyo siyo nyepesi inahitaji moyo wa kujitoa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!