Wananchi na Mashabiki mbalimbali wa Klabu ya Yanga, wamempongeza na Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake na kuhamasisha Wananchi kushiriki zoezi la Sensa.
Wakiwa katika maeneo mbalimbali ya Uwanja wa Taifa, katika kusherehekea Kilele cha Wiki ya Wananchi, mashabiki hao wa Yanga, wameonesha utayari wao kushiriki zoezi la Sensa huku wakiwataka wananchi wengine kuitikia wito wa Rais Samia kushiriki Sensa.