Home Kitaifa MASAUNI, IGP WAMBURA WAAHIDI UCHAGUZI HURU

MASAUNI, IGP WAMBURA WAAHIDI UCHAGUZI HURU

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaahidi watanzania kuwepo kwa Uchaguzi Huru na Haki ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani huku ikisisitiza kila mtu atapata haki yake ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuwepo kwa vihatarishi vya amani katika maeneo yote ambapo chaguzi hizo zitafanyika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akihojiwa na waandishi wa Habari baada ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma huku akisisitiza kuboreshwa na kuwepo kwa ongezeko la bajeti ambalo halijapata kutokea ambapo kikao hicho kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.

‘Niwahakikishie wananchi tumejipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani, niwaombe watanzania watege masikio kuelekea bajeti ya wizara ambayo tutaiwasilisha bungeni katikati ya mwezi unaokuja, tunaenda kuboresha takribani kila sehemu katika vyombo vyetu vya usalama hasa Jeshi la Polisi tunaenda kuliboresha katika kila sehemu ikiwemo vifaa na mambo mengine mbalimbali.’ Alisema Masauni

Akizungumzia zaidi uchaguzi Waziri Masauni amesema wananchi wasiwe na wasiwasi serikali kupitia vyombo vya usalama kupitia Jeshi la Polisi iko vizuri kwa namna yoyote ile kuhakikisha kwamba demokrasia inaendelea kutekelezwa katika misingi ya amani na utulivu,watu wanachagua na kuchaguliwa bila bughudha yoyote nan chi itaendelea kubakia salama katika maeneo yote.

Akizungumzia Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amesema amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kwa kusimamia ongezeko la bajeti kwa wizara na vyombo vyake ambapo ongezeko hilo linaenda kuboresha utendaji kazi hasa wa jeshi la polisi kuelekea pia uchaguzi wa Serikali za Mita ana Uchaguzi Mwakani.

‘Mwaka huu tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi na mwaka kesho uchaguzi mkuu,wizara yetu ina nafasi kubwa sana kuhakikisha uchaguzi unakua wa huru na wa haki kwahiyo niwaombe wajumbe kutambua kwamba hii ngoma bado ni ya kwetu na mpiga ngoma ni Mheshimiwa Waziri kwahiyo tukae tayari kucheza ngoma hiyo ili kuhakikisha chaguzi zote mbili zinapita salama’ alisema IGP Wambura

Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu ambapo mambo mbalimbali kuelekea Bajeti Kuu ya Wizara itakayowasilishwa bungeni katikati ya mwezi ujao yalijadiliwa huku Katibu Mkuu akiwataka watumishi kuwa wabunifu, waadilifu na kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani ya utolewaji wa huduma sahihi na zisizo na upendeleo kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!