Na Boniface Gideon, TANGA
Msimu mpya wa Maonesho ya Biashara yanayohusisha Wajasiriamali wanawake mkoani Tanga maarufu TANGA WOMEN GALA yamezinduliwa Rasmi Jana Juni 24 na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa.
Kwa mujibu wa waandaji wa Maonesho hayo kampuni ya Five Brothers Entanglement nikwamba , maonesho ya mwaka huu yatafanyika rasmi Septemba 27 Hadi 30 nakuhusisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa yote Nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Nasoro Makau aliwaambia Wadau na Waandishi wa Habari kuwa Maonesho hayo mwaka 2023 yanaingia msimu wa 6 tokea kuasisiwa kwake,
“Huu ni msimu wa 6 tokea kuasisiwa kwa Maonesho haya, hii ni fursa kubwa kwa Wajasiriamali na Wafanyabiashara wanawake kutangaza Biashara zao na tunatarajia kupata Wafanyabiashara wakubwa kupitia Maonesho haya na wapo ambao Tayari wameshatoka kupitia Maonesho haya” Alisema Makau
Awali akizindua Maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliwataka Wajasiriamali watumie maonesho hayo kama sehemu ya kutangaza Biashara zao na sio ya kufikiria ya kuuzia tu Biashara .
“Miongoni mwenu mkifika kwenye maonesho mnafikiria kuuza mzigo mlionao kwa siku hizo za maonesho, mkimaliza mnasema faida mmepata mwisho wa siku mnaendelea na maisha mengine” Alisisitiza Mgandilwa
“Tanga Women Gala ni Jukwaa la Wajasiriamali ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuhakikisha wanakua na kuinuka kiuchumi kwa kupanua wigo wa kuwakutanisha linaloandaliwa na Kampuni ya Five Brother Intertainment”
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wabadilike na kuondokana na hali hiyo badala yake watumie kama jukwaa la kutafuta masoko muda wote kwa kujikita kutangaza Biashara zao na sio kuuza tu wakati wa maoyesho.
Alisema kuwa anamatumaini makubwa kwamba katika msimu huo wa sita wa Tanga Women Wajasiriamali watakwenda kutengeneza historia kubwa ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kuwainua wajasiriamali mkoani humo kukua kiuchumi
“Niwashukuru Tanga Women Gala kwa kazi kubwa mnaoendelea kuifanya tunajua inawezekana wakawa hawana cha kuwalipa lakini dua za wajasiriamali ambao kila siku mnaendelea kuwainua ndio malipo yenu” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
“Pamoja na Pongezi mimi kama DC wenu niwapongeza kwa mchango wenu kwa jamii ya wana Tanga ni mkubwa serikali yetu imetengeneza fursa nyingi ikiwemo kutoa wigo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kufanya biashara zao vizuri bila changamoto zozote niliona kama kiongozi wa wilaya niwapongeza niwatake muendeee kufanya hivyo hivyo siku zote” Alisema
Hata hivyo aliwataka kuendelea kupanua wigo kwa wajasiriamali ambao kimsingi hawana uwezo wa kufika kwenye maeneo yao kwa kutengeneza utararibu wa namna ya kuweza kuwafikia na kuwatambua ili kuona namna ya kuwasaidia.
“Lakini maonyesho yetu ni ya siku chache ni vema tukajikita kutengeneza masoko baada ya maonyesho sio wakati wa maonyesho ninasema hivyo kwa sababu kwenye wakati huo tunakuwa na siku tatu mpaka tano hivyo tunapaswa kutegeneza kuona mjasiriamali anafanya biashara siku zote za mwaka” Alisema Mgandilwa