Home Kitaifa MANISPAA YA MUSOMA YAWATAKA WAJASIRIAMALI KUJIANDAA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10

MANISPAA YA MUSOMA YAWATAKA WAJASIRIAMALI KUJIANDAA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE, vijana na wenye ulemavu wajasiriamali wametakiwa kujiandaa na mikopo ya asilimia 10 itakayoanza kutolewa kwa utaratibu mpya.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Meya wa halmashauri ya manispaa ya Musoma, Naima Minga alipozungumza na Mzawa Blog mara baada ya kumaliza kuongoza kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne.

Amesema katika kipindi hiki ambacho serikali inaandaa utaratibu mpya ni vyema wahusika wa mikopo hiyo wakajiandaa ikiwa ni pamoja na kuunda vikundi.

Naima amesema serikali ina nia njema kuhakikisha walengwa wanapata mikopo kwa utaratibu mzuri tofauti na mwanzo ilivyokuwa ikitolewa bila utaratibu mzuri.

Naibu Meya huyo amesema madiwani kwenye Kata zao waendelee kuhamasisha uundwaji wa vikundi ili zoezi la utoaji mikopo litakapoanza liwakute wapo tayari.

“Suala la mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri inafanyiwa maboresho na itakuja kwa utaratibu mzuri hivyo wajasiriamali wanapaswa kujiandaa”

“Katika kipindi hiki ambacho utoaji mikopo umesimamishwa kwa muda kwaajili ya utaratibu mpya walengwa wanapaswa kujiandaa”, amesema Naima.

Katika ukusanyaji wa mapato ya ndani Naibu Meya huyo amesema halmashauri ya manispaa ya Musoma inaendelea kuweka mazingira mazuri ya ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo.

Amesema mapato ya ndani yakikusanywa vizuri yatawezesha kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za utoaji wa mikopo ya asilimia 10.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!