Home Michezo MANDONGA RAUNDI 6 ZA BAIKOKO KESHO NANGWANDA MTWARA

MANDONGA RAUNDI 6 ZA BAIKOKO KESHO NANGWANDA MTWARA

Na.Khadija Seif, Mtwara 

BONDIA wa Ngumi za kulipwa Karim Mandonga atamba kumchezesha mpinzani wake Baikoko , Salim Abeid katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara septemba 24 mwaka huu kuelekea pambano la “Ubabe Ubabe 2” kati ya Twaha Kiduku dhidi ya mpinzani wake Abdo Khaled kutoka Misri.

Akizungumza mara baada ya kupima Afya na kumaliza maandalizi ya mwisho kabla ya kupanda ulingoni kwa Mabondia mbalimbali katika stendi ya zamani Mkoani Mtwara, Bondia wa Kitaifa Twaha Kassim “Kiduku” amesema amejiandaa vizuri kupanda ulingoni dhidi ya mpinzani wake Abdo Khaled kutoka Misri pambano la uzani wa super Middle raundi 10 Huku Kiduku akihaidi kuwapa ushindi watanzania mapema tu na kunyakua mkanda wa UBO.

Hata hivyo nae Bondia kutoka Morogoro mwenye tambo na kipenzi cha watanzania kwa sasa Mandonga “Mtu kazi” ameendeleza tambo zake kuwa yuko tayari kumchezesha mpinzani wake Baikoko mbele ya ulingo na watanzania wasubiri Mandonga akifanya maajabu yake.

Mabondia Wengine watakao panda Ulingoni usiku wa kesho Fransic Miyeyusho dhidi ya Adam Lazaro, Karim mandonga mtu kazi na Salim Abeid, Nasra Msami na Halima Bandora,Osama Arabi wa mtwara na Emilian Polino kutoka JKT huku Pambano kuu Twaha kiduku na Abdo Khaled kwa raundi 10 Katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!