Na Mwandishi Wetu.
Disemba 15, 2023 Luhuvilo Magombola Mkazi wa Mabibo, David Bombeki mwanachuo DIT, na Janeth Emmanuel Mghweno Mkazi wa Shekilango Dar Es Salaam wameingia kwenye Orodha ya Washindi wa Mamilioni ya Fedha kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa , Luhuvilo na David wameshinda Milioni Moja Moja na Janeth ameshinda Milioni Tano ambapo washindi hawa wanaingia kwenye Orodha ya Washindi 50 Hadi hivi sasa wa Kampeni hii.
Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi mfano wa Hundi washindi hawa Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha amewasisitiza Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea
” Muda huu tunaozungumza kuna washindi 15 wanarudi Leo hii kutoka DUBAI, na wengine wamerudi jana kutoka Zanzibar lakini bila kusahau kuna wengine wamejishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” alisema Mary Rutha .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washindi wameipongeza tigo kwa kuwakumbuka wateja wake kupitia kampeni mbalimbali, Aidha wamewasihi watanzania kufanya miamala na Tigo Pesa maana ndo Siri pekeee ya Ushindi.