Home Kitaifa MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) YATOA RAI KWA WAKULIMA KUPATA ELIMU YA...

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) YATOA RAI KWA WAKULIMA KUPATA ELIMU YA KODI

Na Monica Sibanda, Dodoma.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea Nzuguni, Dodoma, ili kupata elimu ya kodi na kufahamu bidhaa za kilimo zilizo kwenye msamaha wa kodi.

Afisa msimamizi wa kodi, Philip Eliamini, ametoa wito huo leo, Agosti 2, 2024, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Eliamini alisema kwamba wamejikita katika kutoa elimu ya kodi kwenye maonesho hayo kwa sababu wakulima ni wadau muhimu wa kodi, na serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kuwawezesha wakulima kulima kibiashara na kulipa kodi.

Nawasihi wakulima wafike kwenye viwanja hivi ili waweze kujifunza na kupata elimu ya msamaha wa kodi kwa dhana za kilimo zilizopo kwenye msamaha huo,” alisema Eliamini.

Mbali na hayo, Eliamini alisema TRA pia inatoa huduma ya namba ya mlipa kodi (TIN) kwa watu ambao hawana, na huduma ya ukadiriaji kodi kwa wafanyabiashara. Pia alibainisha kuwa kila mfanyabiashara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa kutumia mashine ya EFD.

Aidha, Eliamini aliongeza kuwa maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Profesa Shemdoe, yatafanyiwa kazi na wadau wanashauriwa kuyazingatia. Alisema wadau wanaoagiza bidhaa zilizo kwenye msamaha wa kodi wanapaswa kuwasilisha nyaraka zao kwa TRA mapema kabla ya bidhaa hizo kufika. Pia aliwataka watendaji wa TRA kufanya kazi kwa bidii na weledi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!