Baada ya kusambaa kwa taarifa na malalamiko kuhusiana na moja ya wananchi aliyetambulika kwa jina la Bi.Ngorkisho Lowassa Songopa kuwa hajalipwa fidia ya maendelezo na motisha mara baada ya kukubali kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekanusha malalamiko hayo na kueleza kuwa mhusika alikubali kuhama kwa hiyari na kufanyiwa uthamini tarehe 01/08/2022, namba yake ya uthamini ni VAL/NCAA/NGR/KRP/083 na alilipwa malipo yake stahiki yeye pamoja na wategemezi wake.
Na kwamba Tarehe 16/01/2024 Mkuu wa Kaya na wategemezi wake walikubali kusaini malipo ya fidia ya maendelezo na motisha na pia walisaini fomu za kisheria za kukubaliana na zoezi la kuhama kwa hiyari na waliondoka rasmi ndani ya hifadhi tarehe 18/01/2024 kuelekea Msomera.