Tabasamu limeanza kurejea kwa Wanafunzi wa Kike Shule ya Sekondari Mubaba iliyopo Biharamulo baada ya Watu mbalimbali kufika Shuleni hapo na Kuwafariji kufuatia Ajali ya Moto iliyotolewa hivi na kuteketeza Mali zilizokuwa katika Bweni la Wasichana hao.
Miongoni mwa walioguswa na Tukio hilo Ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia UWT Mkoa Kagera Bi. Bernadetha Kasabago Mushashu ambaye Ametembelea Shule hiyo mapema Julai 21, 2022 na kuwapa pole Wanafunzi na Uongozi wa Shule.
Mhe. Mbunge Mama Mshashu akiambatana na Mkuu wa Wilaya Mhe. Kemilembe Lwota amepokelewa Shuleni Mubaba na Walimu pamoja na Wanachama wa CCM Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM kata Kaniha, Mara baada ya kuwasili nakukionea madhara yaliyosababishwa na Moto huo, amekabidhi Vifaa na zawadi alizowabebea Wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya pole zake kwao.
Miongoni mwa Zawadi hizo Ni pamoja na Magodoro 40, Daftari (Counter Books) zaidi ya 400, Mikebe (Mathematical Sets) zaidi ya 100, viburudisho pamoja na Pesa Taslimu Sh. Laki Mbili vyote kwa pamoja vikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 2,993,000/=
“..nimefika hapa Kuwafariji na kuwatia Moyo, tunashukuru Kati yenu hakuna aliyepatwa madhara, poleni na endeleeni Kusoma kwa Bidii, Mama Samia anawapenda anawajali na anawapeni pole, najua wapo waliotangulia na wengine watakuja lakini nilichokuja nacho naomba kipokeeni..” Amesema Mama Mshashu.