Home Kitaifa MAMA MARIAM MWINYI AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI YA BIG WIN UINGEREZA.

MAMA MARIAM MWINYI AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI YA BIG WIN UINGEREZA.

Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mariam Mwinyi ameendelea na ziara yake nchini Uingereza inayolenga kutamatisha ukatii na udhalilishaji wa kijinsia

Ziara hiyo ya kikazi iliyoendelea jana tarehe 17 Novemba 2023.

Mama Mariam Mwinyi amekutana na Taasisi ya Big Win inayoongozwa na Dk .Kasete Admasu wenye ofisi zao Uingereza katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Mazungumzo yao wamegusia ushirikiano katika kufanya kazi kwa pamoja eneo la program itakayohusisha ukuaji wa mtoto hususani kinga na ulinzi dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kuwawekea mazingira salama, pamoja na kuimarisha lishe kwa maendeleo ya ukuaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!