Home Kitaifa MAKONDA KUZUNGUMZA NA WAZEE KESHO MUSOMA, KUFANYA MKUTANO WA HADHARA TARIME

MAKONDA KUZUNGUMZA NA WAZEE KESHO MUSOMA, KUFANYA MKUTANO WA HADHARA TARIME

Na Shomari Binda-Musoma

KATIBU wa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda kesho atazungumza na wazee Musoma mjini katika masuala mbalimbali kabla ya kwenda kufanya mkutano wa hadhara wilayani Tarime.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ziara ya kiongozi huyo mkoani Mara, Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo mkoa wa Mara Simon Rubuga amesema maandalizi ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.

Amesema Makonda anatarajiwa kupokelewa leo novemba 13 majira ya saa 9 alasiri wilayani Bunda na kuelekea wilayani Butiama.

Rubuga amesema akiwa Butiama kiongozi huyo ataweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na baadae kuzungumza na familia yake.

Amesema baada ya kutoka Butiama atakuja kupumzika mjini Musoma kabla ya kuendelea na ziara novemba 14 mkoani Mara.

Mwenezi huyo wa mkoa wa Mara amesema kiongozi huyo katika Siku yake ya pili atafanya kikao na Kamati ya Siasa ya mkoa kisha kuzungumza na wazee mjini Musoma kwenye ukumbi wa CCM.

Mara baada ya kuzungumza na wazee hao atatembelea maeneokadhaa ya mji wa Musoma na baadae kuelekea wilayani Tarime kwaajili ya mkutano wa hadhara.

“Niwaombe wanachama wa CCM na wananchi wote kujitokeza kumpokea na kumsikiliza kiongozi huyo kwenye maeneo yote atakayopita”

“Ameamua kuanzia ziara yake kanda ya ziwa tangu amechaguliwa hivyo ni muhimu kujitokeza kumpokea kwa kishindo kama walivyofanya maeneo mengine ambayo ameshapita” amesema Rubuga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!