Home Kitaifa KATIBU MKUU DKT JINGU: ZINGATIENI UZALENDO ILI TUPATE TAKWIMU SAHIHI

KATIBU MKUU DKT JINGU: ZINGATIENI UZALENDO ILI TUPATE TAKWIMU SAHIHI

NA. MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amewaasa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi kuwa wazalendo katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022 ili kuwa na takwimu sahihi zitakazoleta tija kwa Taifa.

Msimamizi wa Mafunzo ya Sensa Kituo cha Yombo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo, Bi. Joyce Zawadi akieleza hali ya mafunzo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu wakati alipotembelea kituoni hapo.

Ametoa kauli hiyo aliwatembelea na kuzungumza na Makarani, Wasimamizi wa Maudhui pamoja na TEHAMA katika Kituo cha Yombo kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Wilaya ya Ubungo tarehe 15 Agosti, 2022.

Washiriki wa Mafunzo ya Sensa ngazi ya Wilaya wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu (hayupo pichani) alipotembelea kituo cha Yombo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 15, 2022.

Alisema kuwa, Serikali imewaamini kuwapa jukumu la kukusanya taarifa hizo hivyo hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa usahihi kwa kuzingatia weledi na uzalendo wa hali ya juu.

“Takwimu ni jambo muhimu, zoezi hili litasaidia kuwa na taarifa sahihi za takwimu zitakazosaidia shughuli za maendeleo, hata kwa wawekezaji na wafanyabiashara wetu ambao watajua namna bora ya kufanya shughuli zao zitakazochagiza katika ukuaji wa uchumi nchini,”Dkt. Jingu

Aliongezea kuwa Serikali imelipa kipaumbeke suala la sensa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kulibeba jambo hilo kwa unyeti wake, maana linategemewa na taifa zima.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mafunzo ya Sensa katika kituo hicho Bi. Joyce Zawadi alimpongeza katibu Mkuu huyo kwa kutenga muda na kuwatembelea huku akiahidi kuendelea kusimamia mafunzo hayo kwa weledi ili kufanikisha nia ya Serikali.

Washiriki wa Mafunzo ya Sensa ngazi ya Wilaya wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu (hayupo pichani) alipotembelea kituo cha Yombo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti

“Hatutaliangusha Taifa wala Mhe. Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan tupo tayari kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya nchi yetu,”alisema Joyce

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akizungumza na makarani, wasimamizi wa maudhui na TEHAMA alipotembelea katika Kituo cha Yombo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya mafunzo kwa kundi hilo katika kuelekea siku ya Sensa tarehe 23 Agosti, 2022

=MWISHO=

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!