Home Kitaifa MAKANGULA: VIONGOZI WA CCM SAIDIENI VIJANA

MAKANGULA: VIONGOZI WA CCM SAIDIENI VIJANA

Viongozi wa CCM ngazi zote ambao ni walezi wa Jumuiya wametakiwa kuendelea kuwasaidia vijana kutekeleza majukumu Yao ipasavyo yakiwemo ufanywaji wa vikao, kuleta ubunifu katika kazi, kubuni miradi, uandishi wa Taarifa na mipango kazi kiujumla,

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Shadrack Makangula katika ziara yake aliyoifanya kata ya ubungo na kimara akiambatana na kamati ya utekelezaji ya wilaya hiyo kwa lengo la kwenda kukagua Uhai wa Jumuiya na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowahusu vijana.

kwasababu Ninaamini uwepo wa mashirikiano yenu mazuri kutaleta Chachu na Hali ya Hamasa Kwa vijana wetu kufanya vyema zaidi na zaidi.” Alisema Makangula

Aidha Makangula amendelea kuwasisitizia viongozi wa UVCCM ngazi zote kuchapa kazi pasipo kuchoka kwakua kazi hizi tuliziomba wenyewe, “ni wajibu wetu kuona na kufanya Kila linalowezekana Kwa maslahi ya vijana wenzetu waliotuamini na chama Cha Mapinduzi kiujumla.” Alifafanua Makangula

Hata hivyo Viongozi hao walipata wasaa wa kuvitembelea vikundi vya vijana wa Boda Boda ( kikundi Cha Urafiki na kikundi Cha Ngomanagwa) ambapo vikundi hivyo Kwa ujumla wake viliweza kupatiwa vyombo vya usafiri vyenye thamani ya shilling Million 15 kwa kila kikundi ambapo zinatokana na Mikopo wa 4% unaotolewa na Manspaa yetu ya wilaya ya Ubungo

Aidha Makangula aliendelea kuwasisitiza vijana waliokwenye vikundi hivyo kuona haja kubwa ya kufanya marejesho kama inavyostahili Ili vijana wengine waweze kunufaika na Mikopo hiyo kiujumla.

Hata hivyo Makangula aligawa vyeti kwa wadau ambao wanaendelea kutoa sapoti Kwa vijana wetu Kwa ngazi ya kata kwenye matukio mbali mbali, “ninatambua wapo wadau wengi wanaotoa sapoti na wanaondelea kufanya hivyo sisi Taasisi ya UVCCM wilaya tumeona ipo haja ya kutoa vyeti hivyo Kwa wadau wa 5 Kila kata kuonyesha kuthamini mchango wao” alisema.

Aidha amewataka viongozi wa kata na matawi kuunda Kamati ndogo ndogo za kurahisisha majukumu “kanuni yetu ya UVCCM Toleo la mwaka 2019 inaeleza na kutambua umuhimu Mkubwa wa uundwaji wa Kamati hizo ndogo ndogo ambazo kimsingi zitakuwa zinawajibika katika Mabaraza yenu, Hivyo ni wajibu wenu viongozi kuunda kamati hizo iliziweze kusaidia utekelezaji wa majukumu” alisema Makangula

Sanjari na hayo viongozi mbali mbali wa UVCCM waliendelea kusisitiza kwenye maeneo ya kujitegemea, kutengeneza Mahusiano, na kutumia mitandao ya kijamii Kwa kuanzisha page za social media za UVCCM Kwa ngazi zote ili ziweze kuchagiza upatikanaji wa Taarifa na kazi za Jumuiya zinazofanywa kwenye maeneo tofauti tofauti.

Kwa upande wake katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Nehemiah Philemon amewataka vijana na viongozi kupendana na kushirikiana katika shughuli mbali mbali, “Vile vile ni lazima ndugu Viongozi kufanya kazi Kwa kufata miongozo, taratibu, kanuni na Katiba ya CCM kiujumla wake.” Alisema

ziara hiyo ilikuwa na Viongozi mbali mbali katibu wa UVCCM wilaya, katibu wa uhamasishaji na chipukizi, Mwenyekiti wa chipukizi wilaya, Wawakilishi, wajumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM mkoa, wabaraza wa wilaya na mkoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!