Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 14 Januari 2024 amewasili nchini
Uswisi ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa
Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) utakaofanyika tarehe 15 hadi 19 Januari 2024 katika mji wa Davos.
Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya uchumi na uwekezaji, utawala bora, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kilimo.
Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais atafanya mazungumzo ya uwili na viongozi wa mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara