Home Kimataifa MAKAMU WA RAIS AWASILI MISRI KUSHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA AfDB

MAKAMU WA RAIS AWASILI MISRI KUSHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA AfDB

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 22 Mei 2023 amewasili katika mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 Mei 2023.

Mkutano huo unajumuisha Mkutano wa Mwaka wa Baraza Kuu la Benki ya Maendeleo ya Afrika na Mkutano wa 49 wa Mfuko wa Maendeleo ya Afrika chini ya kauli mbiu ya “Kuhamasisha Ufadhili wa Sekta Binafsi kwaajili ya Maendeleo ya Kijani Barani Afrika

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili namna Afrika inavyoweza kutumia sekta binafsi katika kutekeleza ajenda ya mabadiliko ya tabianchi ili kufanikisha lengo lake la maendeleo jumuishi ya kijani.

Mkutano huo unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali, Mawaziri wa Fedha, Magavana, Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Sekta Binafsi pamoja na Wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!