Home Kitaifa MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA CG WA TRA KUJADILI MASUALA YA KIKODI

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA CG WA TRA KUJADILI MASUALA YA KIKODI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Philip Isdor Mpango jana tarehe 27.12.2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda Mayamaya Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuongeza ufanisi wa TRA katika kukusanya Kodi Pamoja na kuondoa ukwepaji kodi nchini ambao umekuwa ukiikosesha Serikali mapato.

“Katika mazungumzo yetu tumepata wasaa wa kujadiliana na Makamu wa Rais namna bora ya kuongeza ufanisi katika kukusanya Kodi na jinsi ya kuondoa suala la ukwepaji wa Kodi” Ameeleza CG Mwenda.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!