Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii. Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.