Home Kitaifa MAKAMPUNI YA CHAKULA CHA MIFUGO YATAKIWA KUWASHIKA MKONO WAFUGAJI KUKU.

MAKAMPUNI YA CHAKULA CHA MIFUGO YATAKIWA KUWASHIKA MKONO WAFUGAJI KUKU.

Na Mariam Muhando- Pwani.

Makampuni ya chakula cha Mifugo Nchini Wametakiwa kujitokeza katika kuwaunga Mkono Wafugaji ili waweze kujikwamua Kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni inayojihusisha na Utatuzi wa changamoto za Wafugaji SAB Saida Bwanakheri katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Wafugaji Kuku yaliofanyika Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani

Mkurugenzi huyo amesema Wafugaji hao wanatakiwa kusaidiwa kwasababu ndio wateja wakubwa wa ununuzi wa Chakula Cha Migugo.

“Nimeona Wafugaji ndio chachu ya Maendeleo yetu hivyo tujitoe kwao kwani Soko letu linazidi kutanuka kwasababu yao hivyo badala ya kumuuzia mifuko miwili ya Chakula ataweza kununua mifuko mingi zaidi,” amesema Saida.

Wakati huo huo amewataka Wananchi wa Wilaya hio kuendelea kujitokeza katika kupata Elimu ya Ufugaji kuku wa Kisasa ili waweze kujikwamua Kiuchumi.

Amesema hali ya hewa ya Kisarawe inaruhusu Ufugaji kwani maeneo yapo mengi hivyo Viongozi wa Kisarawe wako Tayari kuwashika mkono katika kupata fursa hio.

“Sisi SAB tunawaahidi Wananchi wa Kisarawe kupata Tuzo ya Ugaji kuku kwani Kisarawe imekua ikuchukua Tuzo ya Ufugaji N’gombe tu lakini msimu ujao tutakwenda kuendelea kuiheshimisha katika masuala ya Ufugaji kuku pia,” amesema Saida.

Nao Baadhi ya Wananchi walioshiriki Mafunzo hayo Wameishukuru Kampuni hio Kwa kuwafungulia milango katika kujikwamua Kiuchumi kwenye kupata Elimu ya Ufugaji wa Kuku Kwa njia ya Kisasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!