Home Kitaifa Makala aitaka NEMC kutoa Elimu zaidi juu ya madhara mlio Mkubwa kwenye...

Makala aitaka NEMC kutoa Elimu zaidi juu ya madhara mlio Mkubwa kwenye miziki

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameitaka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutowafungia biashara wenye kumbi za Miziki na Burudani kwa kuliza miziki sauti ya juu bali watoe elimu zaidi kuhusu madhara yake.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na kundi la wafanyabiashara wa baa na kumbi za miziki ambao hivi karibuni walitozwa faini za hadi milioni tano na kuzuwa malalamiko toka kwa kundi hilo kuwa adhabu hiyo ni kubwa.

Makalla aliwataka wafanyabiashara hao kufuata sheria za NEMC na hivyo waendelee kufanya biashara zao kwa kutowabughudhi wengine kwa milio mikubwa ya sauti.

“Nawaomba NEMC kaeni na wafanya biashara hao mjadiliane namna ya ulipaji faini kwani kumfungia mtu hataweza kulipa faini vilevile endeleeni kutoa elimu” alisema Makalla.

Alisema serikali inathamini mchango wa wafanyabiiashara kwenye ulipaji wao wa kodi na tozo mbalimbali hata hivyo alisema wasiendeshe shughuli kinyume cha utaratibu.

Awali wafanyabiashara hao walifika kwa maandamano kwenye ofisi ya mkoa wa Mwanza wakiwa na jumbe mbalimbali za malalamiko yao kuwa faini walizotozwa zinazidi mitaji yao hivyo kuitaka serikali kuwaondolea.

Wafanyabiashara hao walisoma risala yao iliyolezea kuwa wametozwa faini kubwa, wakaomba NEMC iendele kutoa elimu kwao na kutokufuatwa kwenye biashara zao na nguvu ya dola.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Mkoani Mwanza Patrick Masagati alisema kuwa wanashukuru usikivu wa serikali katika shughuli wanazofanya hivyo kuahidi kutokuendesha shughuli zao kinyume cha utaratibu na sheria za NEMC.

Aliiomba NEMC kuendelea kutoa elimu kwao ili kuwawezesha kufahamu kiwango cha sauti kisichotakiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!