Home Michezo MAJENGO UNITED MABINGWA MACHUPA SUPER CUP 2022

MAJENGO UNITED MABINGWA MACHUPA SUPER CUP 2022

Na Boniface Gideon, TANGA

Kilele Cha Mashindano ya mpira wa Miguu Jijini Tanga Machupa supper cup yamehitimishwa Jana Disemba 27 kwa Timu ya Majengo United kutawazwa Mabingwa wa Michuano hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 walioupata mbele ya Vijana wa Tallent FC walipokutana kwenye fainali ya kutamtafuta Bingwa atakayeondoka na zawadi ya Ng’ombe, Kombe na jezi katika michuano hiyo iliyofanyika kata ya Duga jijini Tanga.

Fainali hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Magomeni ilikuwa ni bahati yao Majengo United baada ya kuchomoa goli dakika ya 89 ya mchezo walilokuwa wametanguliwa na wapinzani wao mapema kabisa mwa kipindi cha pili hivyo ufundi wa kupiga mikwaju ya penati ukawakosesha Tallent Ubingwa huo.

Licha ya timu ya Tallent kupoteza Ubingwa wa michuano hiyo lakini wamejikusanyia zawadi nyingi zaidi ukiachana na zile za mshindi wa pili ambazo ni jezi seti moja na mipira mitano , wakiongoza kwenye timu yenye nidhamu, Kipa bora Haruna Ally , Kocha Bora Seleman Hamis Mchezaji bora Sadick Abubakary wote hao wametokea timu yao huku kipa bora Ruga Ally akitokea kwa mabingwa Majengo United na Said Danga akitangazwa kuwa ndiye muamuzi bora wa mashindano hayo.

Akizungumza mara baada ya michuano hayo mdhamini wa ligi Thomas Daffa alisema kuwa baada ya kupata wazo la kuanzisha ligi za ndondo aliangalia ni wapi waandaaji wengi wanakwama ili naye aboreshe na alifanikiwa kwa namna yake akiwavuta na kuwashawishi wana michezo wadau na wapenzi wa soka jijini Tanga ambao anaamini watakuwa wamejifunza kitu cha utofauti kutoka kwake kupitia ligi hiyo hukua akiahidi kwa mwaka 2023 kuja kivingine zaidi ya hapo.

“Siku zote ukitaka kuboresha ni lazima kuangalia mapungufu ya wengine , wameanzisha ligi wengi nmeangalia kipi ambacho wao hawafanyi mimi nifanye lakini pia nilitaka kuheshimisha michezo ya ndondo ambayo imeonekana kama michezo ya kihuni lakini nimeweka mashindano haya yakiwa na tuzo mbalimbali inawezekana ni ndondo Cup ya kwanza ndani ya jiji la Tanga kuwa na aina hii ya tuzo nyingi zaidi na mwakani Mungu akitujalia uzima ninakuja kuboresha zaidi ya hapa” alisema Daffa.

Awali akizungumza Ofisa Michezo wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Michael Njaule alimpongeza muandaaji na mdhamini mkuu wa logi hiyo Thomas Daffa kwa namna ambavyo michuano hiyo iliteka hisia za wapenda soka kutoka viunga mbalimbali wa jiji hilo akiwataka wadau kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanyika katika sekta ya michezo ili kuinua vipaji vilivyopo kwa vijana na hatimaye kuweza kuonekana.

“Tunamshukuru na kumpongeza sana ndugu yetu Machupa kwa kuja na wazo la michuano hii wenyewe tumeshuhudia jinsi gani ligi ilivyokuwa ni ukweli usiopingika kuwa vijana wamecheza mpira safi na vipaji tumeviona ni jambo la mfano na kuigwa na wadau, wapenzi soka ili kuweza kuinua michezo na kutangaza vipaji viweze kuonekana” alisema Njaule.

Fainali hizo ambazo ni kwa mara ya kwanza kufanyika ndani ya jiji la Tanga zilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa mziki wa singeli pamoja bongo fleva Seif Shaaban almaarufu kwa jina la Matonya ambaye alivuta hisia za Wananchi kuja kushuhudia kandanda safi ikitembezwa na Vijana waliojaaliwa vipaji na Ufundi mwingi miguuni.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!