Home Kitaifa MAJALIWA: RAIS DKT. SAMIA ANATEKELEZA ILANI KWA VITENDO

MAJALIWA: RAIS DKT. SAMIA ANATEKELEZA ILANI KWA VITENDO

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwatumikia wananchi na kwamba ilani ya uchaguzi ya 2020 inatekelezwa.

Chama kipo imara na kinaendelea kuwatumikia wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ambayo inatekelezwa kwa mafanikio makubwa, hivyo kila Mkuu wa Idara aone kilichoandikwa kuhusu eneo lake na atengeneze mpango kazi wa kuyatekeleza yaliyoahidiwa kwenye ilani hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Februari 4, 2023) wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 46 ya CCM Mkoa wa Kigoma. Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Umoja wilayani Kasulu.

Amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita, Mheshimiwa Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM Taifa amefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali zikiwemo uchumi, elimu, afya, maji, miundombinu, nishati, utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuwa kivutio cha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali, ambapo amesema namna pekee ambayo Watanzania wanaweza kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ni kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema mbali na kuimarisha sekta hizo, Mheshimiwa Rais Samia anaendelea kuimarisha Muungano pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma nchini ili waendelee kuwatumikia wananchi katika maeneo yote.

Awali, Mheshimiwa Waziri Mkuu alizindua ugawaji wa kadi za kielektroniki kwa mkoa wa Kigoma kwa kugawa kadi hizo kwa wanachama wapya 400 wa CCM wa wilaya ya Kasulu. Katika maadhimisho hayo Mkoa umefanikiwa kupata wananchama wapya 2,162 waliojiunga na Chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!