Home Afya MAJALIWA: MSINUNUE DAWA NA KUNYWA BILA KUPIMA

MAJALIWA: MSINUNUE DAWA NA KUNYWA BILA KUPIMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakumbusha Watanzania kufanya vipimo mara wanapobaini kuwa na homa, badala ya kujinunulia dawa na kunywa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Aidha, amewataka Watanzania kuzingatia njia za kujikinga na ugonjwa Malaria ili kupunguza kiwango cha maambukizi na hivyo kufikia lengo la Serikali la kutokomoza kabisa ugonjwa huo.

“Naomba niwakumbushe Viongozi wa Serikali za Mitaa muhakikishe mnasimamia vyandarua vilivyokusudiwa kutumika kujikinga na Malaria havitumiki kufunikia bustani.” Ameagiza Waziri Mkuu

Kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti na Kutokomeza Malaria, vifo vitokanavyo na Malaria nchini vimepungua kwa asilimia 76 kutoka vifo 6,311 mwaka 2015 hadi vifo 1,502 mwaka 2022 huku waliothibitishwa kuugua Malaria wakipungua kutoka watu milioni 7.7 mwaka 2015 hadi watu milioni 3.5 mwaka 2022.

Nayo maambukizi ya Malaria nchini yamepungua ambapo mwaka 2008 takwimu zilionesha kuwa asilimia 18.1 walikuwa na Malaria ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2022 ambapo kiwango kilikuwa asilimia 8.1.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa mwaka huu ni ‘Wakati wa Kutokomeza Malaria ni Sasa Badilika, Wekeza, Tekeleza – Ziro Malaria inaanza na Mimi’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!