Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Disemba 15, 2023 amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ivato uliopo Antananarivo nchini Madagascar na kupokelewa na Waziri Mkuu wa Madagacar, Christian Ntsay.
Mheshimiwa Majaliwa kesho Disemba 16, 2023 atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za kumwapisha Rais wa nchi hiyo, Andry Rajoelina kwenye uwanja wa Mahamasina Barea Stadium.
Mheshimiwa Rajoelina ameshinda nafasi hiyo kwa muhula wa tatu kwa asilimia 58.9 ya kura zilizopigwa akifuatiwa na Siteny Randrianasoloniaiko ambaye alipata kura 14.39.