Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ametembelea wilayani Kilombero kujionea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na changamoto ya mafuriko ili kuchukua hatua
Akitoa taarifa ya mafuriko hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima ameomba Serikali kuwaongezea nguvu kurejesha mawasiliano ya barabara kutoka Ifakara hadi Mlimba pamoja na kurejeshwa mawasiliano ya njia ya reli ya Tazara ambayo nayo yamekatika kabisa.
Aidha mkuu wa Mkoa ameiomba Serikali kuwapatia usafiri helikopta ili kuweza kufikisha chakula kwa wananchi wa kata mbili za Masagati na Utengule ambao hadi sasa wapo kisiwani.