Home Kitaifa MAJADILIANO YA UPATIKANAJI KATIBA MPYA BADO KUFIKIA MUAFAKA

MAJADILIANO YA UPATIKANAJI KATIBA MPYA BADO KUFIKIA MUAFAKA

Na Magrethy Katengu

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbalo amefungua Kikao cha Mawaziri wa Sheria na wanasheria Wakuu wa serikali Wastaafu na waliopo madarakani kuhusu Majadiliano ya Mchakato wa katiba Mpya pamoja na Mkakati wa elimu ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Akizungumza wakati akifungua kikao hiko leo Jijini Dar es salaam amesema lengo nikujadili mchakato wa katiba mpya pendekezwa ambapo mchakato huo ulianza 2014 na bado haujafukia muafaka wa kuanza kwa katiba mpya

Hata hivyo Dkt. Ndumbaro amesema kikao hiko kitajenga Uelewa na kutoa Elimu juu ya Mwenendo wa mchakato wa katiba mpya.

Zaidi ya Asilimia 50 ya Watanzania hawafahamu mapungufu yaliyopo katima katiba ya zamani ya mwaka 1977 hivyo wanaofahu hutoa elimu na kuomba watoe mapendekezo yao ili iwe faida kwa jamii yote kwa ujumla “ amesema Waziri wa katiba na Sheria Dkt. Ndumbalo.

Majukumu ya wizara ya katiba na sheria ni kuratibu mchakato wa katiba ya mwaka 1977 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mawaziri wastaafu wanasheria na wale waliopo madarakani kupata mlengo mmoja uliokusudiwa

Nimefungua kikao hiki Leo ili kupitia kikao hiki tutapata maoni yenu kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara kufahamu wapi kulitakiwa kufanyiwa marekebisho katika ya 1977 ” . Dkt. Ndumbalo.

Naye aliyewahi kuwa Waziri wa katiba na sheria Mery Nagu amesema ujio wa katiba ni muhimu sana kwa Taifa kama la Tanzania linalopiga hatua kiuchumi na kisiasa kwani kuna baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopo kwenye rasimu ya 1977 vunahitaji vifanyiwe marekebisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!