Na Scolastica Msewa, Kigamboni
Waziri wa nchi katika Ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Selemani Jaffo amesema maisha ya mwanadamu yanategemea utunzaji wa mazingira ili kuwa na kizazi endelevu hivyo ameitaka jamii kupanda miti na kutunza mazingira.
Amesema hayo Kigamboni akiwa amewakilishwa na Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Temeke Arnold Mapinduzi wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo Ofisi ya usimamizi wa utunzaji wa mazingira TEEMO ilizinduliwa.
Alisema uhai na uendelevu wa binadamu na viumbe wengine hutegemea utunzaji bora wa mazingira tunazungumzia uhai endelevu kati ya binadamu na viumbe hai vingine vinavyoendeleza uhai wa binadamu.
Jaffo alisema binadamu na viumbe vitakosa hewa ya kupumua, vitakosa maji salama ya kunywa na matumizi mengine hata mpaka viwandani ikiwa ni pamoja na kukosa chakula safi na salama na ardhi nzuri na salama ni yule anayeishi kwenye ardhi iliyokosa afya ya udongo.
“Afya ya udongo ikiathirika hata vyakula hatutapata kwasababu kinachozalisha ni ardhi hii kwani kule kwenye ardhi Kuna viumbe ambavyo havionekani ambao wanakazi ya kurutubisha udongo hapo hata ukidumbukiza kitu kinachooza hakitaoza na mzunguka wa hewa hautafanyika tutakuwa tumeiua ardhi na tutakuwa tumejiua sisi wenyewe” alisema Jaffo.
Alisema mtu wa mwisho wa kulalamika kuvikosa hivyo vitu ni binadamu kwasababu unapozungumza mazingira bila kutunza mazingira hatuwezi kuona mafanikio yakitimia.
Aidha aliwapongeza Taasisi ya TEEMO kwa jitihada mbalimbali za utekelezaji wa kutunza mazingira ya mji wa Kigamboni na fukwe za bahari ya Hindi.”Namuendelee kupambana katika kutunza na kuhifadhi mazingira yetu.
“Niwapongeze TEEMO kwani na wao wamekuwa wanamazingira katika kutetea uhai endelevu wa binadamu na viumbe wengine duniani ambapo katika kupambana huko Sasa wameweza kuwa na ofisi na Mheshimiwa Waziri Jaffo aliombwa kujakufungua na alikubali kuja kuzindua ofisi yao ambayo nitaizindua baada ya hotuba hii ya kukwakirisha kwaniba yake” alisema Mapinduzi akimwakirisha Waziri Jaffo.
“Mnachofanya TEEMO na Wadau wengine wa kutunza mazingira Kweli nawapongeza sana kwa kutunza mazingira hata kusafishwa fukwe na beach zetu kwani mnapofanya hivyo ukiangalis kwenye sheria zetu hasa ya mwaka 2004 kifungu cha 18 Moja ya jukumu la NEMC ni kutoa elimu na kusaidia kuongeza uelewa kwa watu kazi ambazo hatuwezi kuzifanya peke yetu”
“Wadau kama nyie ndio mnatussidia kuendeleza kwahiyo akinamama na kinababa hongera zenu katika kushiriki utunzaji wa mazingira nchini hivyo muendeleze elimu hii mpaka kwa watoto wenu na kizazi kijacho yaani tuangalie huu uumbaji wa Mungu kwa mapana yake kwa kulinda na kutunza” alisema.
Awali akimkaribisha Mwakirishi huyo wa Waziri Jaffo Mkurugenzi wa Taasisi ya TEEMO na mshauri wa masuala ya mazingira Winfrida Shonde alisema Taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya na kuwezesha jamii katika utunzaji wa mazingira ilikufikisha ajenda ya utunzaji wa mazingira mbele.
Winfrida alisema wanakampeni mbalimbali za utunzaji wa mazingira nchini ikiwemo katika maeneo ya fukwe za bahari ilikuwa na mazingira bora na salama kwa kizazi endelevu.