Home Kitaifa MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAHITIMISHA WIKI YA SHERIA

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAHITIMISHA WIKI YA SHERIA

Mahakama kuu ya Kanda ya Mwanza imeadhimisha maadhimisho ya kilele cha wiki na siku ya sheria mwaka 2023 yenye kauli mbiu isemayo; Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu – wajibu wa mahakama na wadau.

Usuluhishi wa mgogoro unajenga na kuimarisha mahusiano katika jamii ila unapomalizwa mahakamani watu uendelea kuwa na migogoro baina yao ila usuluhishi utatua mgogoro na watu wakaendela kuishi kwa pamoja na ushirikiano, Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Mwanza, Dr. Ntemi Kilekamajenga

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Monica Ndyekobora amesema, siku saba za maadhimisho ya wiki ya sheria moja kati ya migogoro waliyofanikiwa kusuluhisha katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Nyegezi, ni kwa vijana wawili ambao walitaka kuuana baada ya kukopeshana shilingi elfu moja.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Hassan Masala ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kutoa fedha za kujenga na kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu ya mahakama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!