Home Kitaifa MAGARI 30 YA LUMBESA YAKAMATWA PWANI

MAGARI 30 YA LUMBESA YAKAMATWA PWANI

Na Scolastica Msewa, Kibaha
Jumla Kiasi cha shilingi milioni 60 zimekusanywa kutokana na faini za magunia 3128 ya mazao yaliyozidisha uzito wa kilo 100 (lumbesa) katika Barabara kuu ya Morogoro maeneo ya Kibaha Mailimoja na mizani ya TANROADS Bagamoyo zoezi la ukaguzi wa lumbesa la mazao ya shamba lililofanywa na Wakala wa VIPIMO WMA mkoani Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Kibaha mkoani Pwani wakati akitoa taarifa ya operesheni ya ukaguzi wa lumbesa mkoa wa Pwani iliyofanyika kati ya tarehe 10 Hadi 17 mwezi Februari Meneja wa Wakala wa VIPIMO WMA mkoa wa Pwani Hashimu Athumani amesema zoezi hilo lililofanyika wakati wa mchana na usiku ambapo magari 30 yalikamatwa.

Hashimu alisema magari 20 yakiwa na magunia yenye lumbesa yalikamatwa Kibaha Mailimoja na magari 10 yalikamatwa yakiwa na magunia yenye lumbesa katika mizani ya Tanroads Bagamoyo ambapo magunia yalikamatwa na uzito wa zaidi ya kilo 106 hadi kilo 206.

Alitaja aina ya mazao yaliyobebwa kuwa ni pamoja na mahindi, vitunguu maji, viazi vitamu,, mboga mboga, tangawizi, maembe, mapeasi na viazi mvilingo.

“Wahusika wote walikili makosa na kukubali kulipa faini hiyo ya milioni 60 hivyo hakuna aliyefikishwa mahakamani”

Aidha Meneja huyo wa Wakala wa VIPIMO WMA mkoa wa Pwani alisema operesheni hiyo ya ukaguzi wa lumbesa katika mazao ya shamba niendelevu hivyo amewataka wakulima na wafanyabiashara kuzingatia sheria kwa kutofungasha magunia bila kuzidishwa uzito wa kilo 100 katika ubebaji wa mazao yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!