Home Kitaifa MAGANYA, RC MTAKA WAHUDHURIA MAZISHI YA HERMAN KIRIGINI

MAGANYA, RC MTAKA WAHUDHURIA MAZISHI YA HERMAN KIRIGINI

Na Shomari Binda-Butiama

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya na mkuu wa mkoa wa Njombe,Antony Mtaka, wameongoza waombolezaji kwenye mazishi ya Herman Kirigini.

Marehemu Herman Kirigini enzi ya uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na Waziri Kilimo na Mifugo tangu mwaka 1980 hadi mwaka 1985.

Akitoa salamu za rambirambi Maganya ambaye aliongozana na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi na chama amesema yapo mambo ya kujifunza juu ya maisha ya Kirigini.

Amesema katika historia ya uongozi wake Kirigini alikuwa kiongozi ambaye alitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia utaratibu na historia imesema hivyo.

Maganya amesema ipo alama ambayo imeachwa na kiongozi huyo ndani ya Jumuiya na chama na ameacha watoto wanaofuata nyayo zake.

Jumuiya ya Wazazi imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huu wa kiongozi wetu na sisi kama viongozi wa sasa tupo karibu na familia kwa kipindi hiki”,amesema Maganya.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka, amesema hajafanya kazi na marehemu Herman Kirigini lakini amepata ushauri sana kwa kiongozi huyo.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amesema katika kumuenzi Herman Kirigini ni kufuata mazuri yote aliyoyatenda na kwani katika uhai wake alilitumikia jimbo kwa uhadilifu mkubwa.

Amesema familia ya Kirigini ina heshima kubwa tangu enzi za baba mzazi wa Herman Kirigini mmoja wa walimu aliyemfundisha Mwalimu Nyerere hivyo ni muhimu hestoria iseme hivyo.

Mtoto wa marehemu, Peter Kirigini katika wasifu wa marehemu amesema licha ya nafasi ya ubunge na waziri lakini pia marehemu Harman Kirigini, amewahi kushika nafasi ya ukuu wa wilaya ya Meatu na Kiteto.

Aidha Peter amewashukuru madaktari kwa kumuhudumia wakati wa ugonjwa wake pamoja na wananchi kwa kuwafariji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!