
Na Shomari Binda-Musoma
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Fadhili Maganya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla umoja wa jamii ya wana Musoma itakayofanyika ijumaa februari 21
Licha ya Maganya wageni wengine walioalikwa ni mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi,Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka,mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo na viongozi wengine.
Akizungumza na Mzawa Blog kuelekea hafla inayowakutanisha wana Musoma kwaajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya kijamii,Mwenyekiti wa umoja huo Benedict Magiri amesema maandalizi yote yamekamilika.
Amesema wamemuomba kiongozi huyo kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo wakiamini atawaachia ujumbe utakaowajenga
Magiri amesema kiongozi huyo amewakubalia kushiriki pamoja nao wskiwemo wageni mbalimbali waliowaalika
Amesema kwenye hafla hiyo licha ya kukutana masuala mbalimbali yatazungumziwa pamoja na chagizo dogo la kusaidia vifaa vya umoja huo.
Mwenyekiti huyo amewaomba wana umoja kufika kwa wakati kwenye ukumbi wa Mwenbeni complex ili kujumuika kwa pamoja
” Maandalizi ya hafla ya kukutana kwa jamii ya wana Musoma yamekamilika na kila kitu kinakwenda sawa.
” Tunamshukuru mheshimiwa Maganya tumemualika na ametukubalia kushiriki nasi kwenye tukio hili muhimu litakalofanyika ijumaa hii”,amesema.
Aidha Mwenyekiti huyo wa jamii ya wana Musoma amesema mwaka huu wamejipanga vizuri na hafla hiyo huku buridani nyingi zikiandaliwa pamoja na vinywaji na chakula.