
Na Shomari Binda-Musoma
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Fadhili Maganya amewataka wana umoja jamii ya Musoma kuwa na upendo na kushirikiana kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Maganya amesema si vyema kutengenezeana ajali za kisiasa ili kuona mwingine anaalibikiwa kwani kuna maisha yanaendelea baada ya uchaguzi.
Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake usiku wa jana februari 21/2025 na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kwenye hafla ya umoja wa jamii ya wana Musoma.
Amesema upendo na mshikamano utawafanya kuweza kusaidiana kwenye masuala mbalimbali hata kuinuana kiuchumi hivyo wasikubali kutenganishwa na siasa.
Maganya katika ujumbe wake huo amesema mwaka huu ukiwa mwaka wa uchaguzi wana Musoma wasitengenezeane chuki bali wazidishe upendo na kuwapongeza kwa namna walivyoanzisha umoja huo wa kuweza kusaidiana na kufarijiana.
” Hayo ndio niliyoagizwa na Mwenyekiti wetu wa Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) niweze kuwaeleza juu ya upendo na kushirikiana.
” Ni ujumbe ambao unapaswa kuzingatiwa na kila mmoja wetu kwa kuwa upendo unapokuwepo haiwezi kutokea chuki kati yetu”,amesema.

Kwa upande wa ujumbe wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti huyo wa Wazazi amesema amekusudia kuijenga Musoma ya kiuchumi kwa kufungua milango iliyofunga.
Amesema moja ya eneo hilo ni kukamilishwa kwa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Musoma kwa wakati baada ya serikali kulipa fidia wananchi kupisha eneo la upanuzi.
Licha ya kukusudia kuifungua Musoma kiuchumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko la kisasa pamoja na stendi amempongeza Mwenyekiti wa umoja huo kwa kuwaunganisha watu na kutoa ushauri wa kujipanga kabla ya matukio kutokea kuwa na fedha ya kusaidiana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo Magiri Benedict amesema umoja wa jamii ya wana Musoma umeendelea kuimalika na sasa wamekusudia kuongeza ufanisi kwa kuwa na vitendea kazi vitakavyowasaidia kwenye matukio yao.
Katika hafla hiyo ilifanyika chagizo la kupatika viti kwaajili ya umoja huo lengo likiwa viti Mia 500 na kuvukwa lengo kwa kupatikana viti zaidi ya 600 vilivyochangiwa na wana umoja na wadau mbalimbali.
