Home Kitaifa MAFIA NDIO KITIVO CHA MAZALIA YA SAMAKI DUNIANI

MAFIA NDIO KITIVO CHA MAZALIA YA SAMAKI DUNIANI

Mkuu wa kitengo Cha kilimo biashara wa Bank ya NMB makao makuu Nsolo Mlozi amesema Bank ya NMB imefanya mabadiliko makubwa kwa kuanza kutoa uwezeshaji kwa kundi la Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kwa kuwakopesha dhana za Uvuvi, kilimo na ufugaji kwa lengo la kuwainua kiuchumi makundi hayo nchini.

Amesema Sekta ya kibenki ni muhimu katika uhimarishaji wa maendeleo ya nchi yoyote duniani hivyo wameamua kutoa mikopo hiyo kwa Wavuvi, Wakulima na Wafugaji nchini.

Awali akizungumzia mkakati wa serikali kuhakikisha Wilaya ya Mafia inafikika kiurahisi na Wananchi na Watalii Mkuu wa Wilaya ya Mafia Zephania Sumaye amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi billioni kwaajili ya kuleta kivuko kikubwa kipya ikiwa ni pamoja na kuelea na uboreshaji wa uwanja wa ndege Wilaya ya mafia.

Meneja wa Kanda ya Mashariki kusini Lilian KasaAFIA amewataadharisha uongozi wa Wilaya Mafia mkoani katika uwekezaji huo mkubwa wa Sekta ya utalii kwa kuhakikisha wanahimalisha utunzaji wa mazingira ili kuwa na matokeo ya uchumi wa Bluu endelevu.

Amesema uwekezaji huo unaweza kuchangia kuharibu mazalia ya samaki wetu hivyo wote tunawajibu wa kulinda na kutunza mazingira ili tuendelee kunufaika na mazalia ya samaki wetu.
++++++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!