Home Kitaifa MAFIA BOXING YALETA NEEMA KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA.

MAFIA BOXING YALETA NEEMA KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA.

Kampuni ya Mafia Promotion Boxing imetoa misaada ya majiko ya gesi kwa wanawake wanaofanya shughuli za uuzaji wa vyakula katika masoko ya Mgandini, Makorora na Mlango wa Chuma yaliyoko jijini Tanga pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto yatima cha Green Instead Ophanege Foundation kilichopo eneo la Bombo jijini hapa,ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.

Ikumbukwe kuwa mabondia mbalimbali wanaodhaminiwa na kampuni hiyo, walipata ushindi katika mapambano yao walipopanda ulingoni 0ctoba 5,2024 jijini Dar es salaam.
Aidha pambano hilo ambalo lilichagizwa na Technical Knock Out ‘KO ya Mama’ambapo baada ya ushindi huo,Rais Samia alitoa zawadi kwa mabondia hao ambayo imewatia hamasa kuhakikisha wanazidi kuijengea heshima Tanzania kupitia mchezo wa ngumi.

Akizungumza mkurugenzi mkuu wa matangazo na uzalishaji kutoka kampuni ya Mafia Promotion ,Omari Clayton alisema kuwa pamoja kurudisha fadhila kwa jamii ,kama kawaida yao wanaungana na watanzania kupitia kampeni ya Rais Dkt. Samia ya kuhamasisha juu ya matumizi ya nishati safi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni katika kupikia na shughuli nyingine hali ambayo inasababisha mabadiliko ya tabianchi na uzalishaji wa hewa ukaa.

“Kampuni ya Mafia Boxing Promotion tunaunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupambana na kuhamasisha watanzania kuhama kutoka kwenye matumizi ya mkaa na kuni kupikia na kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ndio maana leo tumegawa majiko ya gesi kwa mama zetu wanapika vyakula katika masoko yaliyopo katika jiji la Tanga” alisema Clayton.

“Tumehamasika na tunampongeza sana Rais Samia kwa ‘KO ya Mama’ na kuwazawadia mabodia wetu ambao walipambana kuhakikisha wanabakisha mikanda hapa Tanzania na walifanikiwa hivyo,nasi tunazidi kumuahidi kwamba mama kupitia Mafia Boxing tutazidi kuiheshimisha Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya mabondi wenzanke,Ibrahim Mafia haikuwa alisema rahisi kupamba ulingoni kutokana na mpinzani wake lakini kupitia maombi ya watanzania alipambana kuhakikisha anawapa furaha kwa kupata ushindi ambao alifanikiwa

“Ule ushindi ni ushindi ni ushindi wetu lakini pia ni ushindi wa watanzania ambao walikuwa wakituombea tumepokea zawadi kutoka kwa Rais wetu mama Samia tukaona hatuwezi kuituia peke yetu tukaona tushirikiane kile ambacho tumepata kwa kuwapa majiko ya gesi na kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima tunaomba mzidi kutuombea dua ili wakati mwingine tuweze kutoa kikubwa zaidi. Alisema Mafia”

Ibrahim Mafia ambaye alipanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Enoch Tettey raia wa Ghana kuwania mkanda wa dunia ‘World Boxing Council Bantamweight’ kwenye uzan wa kilogram 53 katika ukumbi wa City Center Hall Magomeni Sokoni na hatimaye kufanikiwa kubwaga chini mpinzani wake kwa njia ya KO.

Wakizungumza baadhi ya waliopata majiko ya gesi,wamewapongeza mabondia wote kwa ushindi walioupata pamoja na kuishukuru Kampuni ya Mafia Boxing Promotion kwa kuwapatia mitungi ya gesi ambayo itawasaidia katika shughuli zao.
“Tunawashukuru sana kwa zawadi zenu na sisi tunaendelea kuwaombea kwa Mungu hakika atawalipa tulikua na changamoto ya kupata mkaa kwaajili ya kupikia lakini sasa kupitia majiko haya yatatusaidia kurahisisha shughuli zetu za kupika kila siku, tunamshukuru sana mama Samia kwa msaada wake wa majiko haya” walisema.

                    MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!