Home Kitaifa Madereva watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani

Madereva watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani

Koplo Rehema Makalla kitengo cha elimu ya usalama barabarani wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza amewataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ilikuepusha ajali zitokanazo na uzembe wa madereva.

Ameyasema hayo wakati akitoa elimu ya usalama barabarani kupitia kituo cha Redio Metro Fm kwenye kipindi cha pambazuko. Aidha Rehema amesema kuwa ajali za barabarani zimekuwa na athari kubwa kwa jamii kwani zimekuwa zikipunguza nguvu kazi kwa taifa.

Katika hatua nyingine Koplo Rehema amebainisha kuwa vyanzo vikubuwa vinavyosababisha ajali ni mwendo kasi kwa madereva, Ulevi, ukungu, mvua kubwa pamoja na ubovu wa miundombinu.

Hata hivyo amewataka madereva kwenda kusomea fani ya udereva katika vyuo vilivyosajiliwa na mamlaka husika nakuacha kujifunza kiholela mitaani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!