Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
ARUSHA-TANZANIA
Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha kuchukuliwa hatua kali za kisheria endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022 katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani.
Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva.
Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa dola.
SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo mbinu.
Sambamba na hilo amesema kuwa chanzo cha ajali nyingi ni ushabiki wa mwendo kasi ambapo amewataka madereva hao kuwapuuza wanaowashawishi kwenda mwendo kasi ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
Kwa upande upande wake Bw. George Emmmanuel ambae ni dereva amelishukuru Jeshi la Polisi husasani kikosi cha usalama barabarani kwa kutoa elimu na kuwa kuwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia Barabarani.