Home Afya MADAKTARI BINGWA WA MACHO KUWEKA KAMBI HOSPITAL YA MWALIMU NYERERE MUSOMA

MADAKTARI BINGWA WA MACHO KUWEKA KAMBI HOSPITAL YA MWALIMU NYERERE MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya madaktari bingwa kutoka hospital ya kanda Bugando wanatarajiwa kuweka kambi ya kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya macho kwenye hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na Mzawa Blog, Mganga mfawidhi wa hospital hiyo Osmund Dyagura amesema lengo la ujio wa madaktari hao ni kuwafikia wananchi katika kuwapa huduma bora za kibingwa.

Amesema madaktari hao watatoa huduma kwa siku 5 kuanzia jumatatu ya agost 14 hadi agost 18 na kutoa wito kwa wananchi kujiandikisha mapema kwaajili ya kupata huduma hiyo.

Dyagura amesema hii ni fursa ya kukutana na madaktari bingwa bila kutumia gharama za kuwafuata hospital ya rufaa ya kanda Bugando na kuwaomba wananchi kuitumia.

Amesema huduma kwa wagonjwa wanaotumia bima za afya watapokelewa kwa kutumia bima zao na kuhudumiwa na wale wasiokuwa na bima watahudumiwa kwa utaratibu wa kawaida wa hospital.

“Hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere dhamira yake ni kuwafikishia huduma bora na za kibingwa wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo mengine”

“Tumekuwa tukipata ujio wa madaktari bingwa mara kwa mara na tumekuwa tukiwatangazia wananchi kufika na safari hii tutakuwa na madaktari bingwa wa macho” amesema Dyagura.

Amesema wananchi wenye matatizo ya macho wapo wengi na madaktari hao wamejipanga vizuri kwa kutumia vifaa bora kuwaona.

Tayari baadhi ya wananchi wameanza kufika hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kujiandikisha kwaajili ya kupata huduma hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!