Home Michezo MABINGWA 50 MTOKO WA KIBINGWA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO KI VIP

MABINGWA 50 MTOKO WA KIBINGWA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO KI VIP

KAMPENI kubwa ya Mtoko wa Kibingwa yazinduliwa rasmi mabingwa 50 kushuhudia derby ya kariakoo katika Jukwaa la VIP A Novemba 05, 2033 Kwa Mkapa.

Akizungumza na Wanahabari Leo oktoba 02, 2023 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa amesema Kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake kwa promosheni mbalimbali ili kuonesha jinsi gani ina wajali wateja wake na wanamichezo kwa ujumla na kufikisha wateja 300 wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu uliopita.

Rugambwa ameeleza kuwa promosheni ya mtoko wa kibingwa msimu wa 06 utakuwa wa kitofauti zaidi ambapo washiriki 50 watapata huduma za malazi ,usafiri pamoja tiketi ya VIP A kwa ajili ya kushuhudia derby hiyo huku zaidi mengine yakibaki kuwa ya surprise ili kuleta utofauti kwa mabingwa wa msimu uliopita.

Aidha amefafanua zaidi kupitia promosheni hiyo imekuwa na muitikio mkubwa sana kutokana na washiriki wengi kutokea Mikoani.

“Kama betika tunapata muitikio mkubw wakuendelea kuwepo kwa promosheni hii kutokana na washindi wengi kutokea mikoani hivyo tunapata muitikio kuwa kampuni imefika mbali zaidi na huduma zinawafikia tunapata mrejesho mzuri wa kampuni yetu kujitangaza.”

Pia amesema mabingwa wabpromosheni hiyo watapatikana kwa njia ya droo ambazo zitafanyika kila wiki siku ya jumanne ambapo rasmi zitaanza oktoba 10,2023 na kufikia kilele chake Oktoba 31,2023.

“Ni rahisi mshiriki anatakiwa kuwa na vigezo vya kushiriki ni pamoja na kubeti mkeka wenye mechi kuanzia 03 na dau la kubeti liwe kuanzia shilingi 2000 au zaidi”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!