Home Michezo MABINGWA 100 WA BETIKA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO     

MABINGWA 100 WA BETIKA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO     

KAMPENI ya Mtoko wa kibingwa yafikia tamati mara baada ya washindi 100 kutoka mikoa yote Tanzania kuwasili Jijini Dar es salaam  kwa ajili ya kutazama Mtanange wa derby ya  Afrika mashariki kati ya Simba na Yanga inayotarajiwa kua kesho kwenye dimba la mkapa.

Akizungumza na Wanahabari  Aprili 15,2023 Uwanja wa ndege Jijini Dar es salaam  wakati wa Mapokezi ya washindi wa mtoko wa kibingwa  Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Betika  Nelson Pius amesema kuwasili kwa washindi hao kunaleta historia ndani a msimu huo wa 5 kutimiza washindi 100 kutoka mikoa mbalimbali huku Mshindi mmoja akiwa Mwanamke kutoka Chamazi Jijini Dar es salaam.

Tayari washindi wetu wamewasili kutoka mikoani ikiwemo Geita,Mtwara,Sumbawanga, Simiyu,Songwe Dar es salaam na sehemu mbalimbali ni furaha yetu kuwa watakwenda kutazama derby ya Kariakoo kama dhamira ya kampuni ya betika ilivyoandaa shughuli hii tangu kuzinduliwa kwa Kampeni awali mwezi Febuari.”

Hata hivyo Pius ameeleza kuwa Washindi hao wamepatikana kupitia droo za kila siku ambapo mshiriki aliweza kuweka ubashiri wake kwa dau la shilingi mia 500 na betika ilimpa nafasi kila anaeweka dau lake kupata nafasi ya kuingia kwenye droo.

Tayari washindi wetu wametuwa dar mapema hivyo kutafatiwa na bata la mtoko wa kibingwa itakayofanyika kidimbwi huku siku ya kesho watasindikizwa na king’ora hadi uwanjani na watapata huduma ya kipekee.

Kwa upande wake Mshindi kutoka Njombe Salivius Lucas Frugence amesema amefurahi kufika Dar es salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia derby hiyo mubashara akiwa na maandalizi ya kipekee huku wakisindikizwa na Msafara wa jeshi la polisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!