Home Kitaifa MABALOZI WA AFRIKA NCHINI KUSHIRIKI MBIO ZA MARATHONI

MABALOZI WA AFRIKA NCHINI KUSHIRIKI MBIO ZA MARATHONI

Na Magrethy Katengu—Dar es salaam

Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wanatarajia kushiriki mbio za riadha kuanzia kilomita 5 hadi 15 zitakazofanyika Mei 18 ,2024

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga leo Mei 15, 2024 Jijini Dar es salaam katika mkutano wa waandishi wa habari na Umoja wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini ambapo amebainisha kuwa katika mbio hizo kutakuwa na makundi mawili kundi la kwanza watakimbia kilomita tano na kundi lingine watakimbia kilomita 15 .

Hata hivyo amebainisha kuwa mbio hizo zitaanzia Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere- Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 12 asubuhi kwa kuanza na kundi la kwanza litalokimbia kilomita 15, kupitia barabara ya Baraka Obama na kuelekea hadi Aga khan na kupita daraja la Tanzanite hadi Masaki na hatimae kugeuza na kurudi JINCC.

Sambamba na kundi la pili watakimbia kilomita tano wataanza saa 12:30 asubuhi na kupitia barabara Baraka Obama na kukimbia hadii Aghakhan hospitali kisha kurudia Ukumbi wa JINCC.

Katika riadha hii tumewalika wakimbiaji mashughi kutoka Tanzania ili kuadhimisha siku hii, ambao wengine ni wakimbiaji walioshinda kwenye mashindano ya riadha ya Olimpiki na tayari wamejisajili ,”alisema.

Balozi Mindi amefafanua kuwa maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Mei 25 ambapo kwa mwaka huu watafanya kwa kushirikiana na kundi la mabalozi wa Afrika, hivyo wameona waadhimishe siku hiyo kwa mbio za riadhaa kwa ajili ya kusherekea Siku ya Afrika.

Aidha riadha hiyo itakuwa sio ya kawaida watu watalipa hela na watajiandikisha lengo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kwenda kusaidia shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zilizopo jijini Dar es Salaam hivyo kitakachopatikana kutokana na riadha hizo basi kitaenda katika hizo shule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!