DC LUSHOTO AWAALIKA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KWENYE SEKTA MBALIMBALI NDANI YA WILAYA HIYO.
Na Ashrack miraji.
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Japhari kubecha ameyasema hayo Katika Kuelekea tamasha la Usambara tourism Festival ambalo linatarajiwa kufanyika 6 – 7 September 2024
Akizungumza na Mwaandishi wetu ofisini kwake DC huyo amesema Wilaya ya Lushoto ni wilaya pekee ambayo imebarikiwa Kuwa na vivutioa vingi vya kitalii na ni wilaya ambayo imebarikiwa Kuwa na rasilimali nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza na kufanya biashara zao za kiuchumi Kwa kushirikiana na serikali Katika kulijenga Taifa letu
Wilaya ya Lushoto imegawanyika Katika Halmashauri mbili ambazo ni halmashauri ya Lushoto na Bumbuli ukizingatia halmashauri ya bumbuli imebarikiwa Aridhi yake Kuwa na madini Mbalimbali ikiwemo dhahabu madin ulanga na bouxite ambayo Kwa wingi wake yanapatika Lushoto wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na rasilimali hizo kujipatia kipato na halmashauri kupata mapato.
“Nitumie fursa hii Kwa Watanzania wote hivi karibu tunakwenda kufanya Tamasha kubwa la kihistoria ambalo tumelipa jina la Usambara tourism Festival kuja kujionea fulsa Mbalimbali ambazo zinapatikana hapa na tutatembea Kwa pamoja kujifunza vitu vingi vya kihistoria Katika wilaya Yetu”
“Sambamba na hayo wawekezaji wa ndani na wa nje mnakaribishwa kuja kuwekeza biashara zenu hapa Lushoto milango hipo wazi kuanzia ofisi ya Mkoa mpaka ya wilaya tutawapa ushirikiano wa kutosha hili kuendelea na shughuli za kiuchumi Katika wilaya yetu”.
“Alisema DC kubecha “.
DC kubecha ameendelea kusema lengo la kufanya Tamasha hili ni kumuunga Mkono Mhe Rais wa jamuhur ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hasa Katika sekta ya utalii yeye amekuwa kinara wa sekta hii tumeshuhudia mapato Mengi na Wageni wengi wanakuja Tanzania kutembelea Utalii wetu kufanya uwekezaji hapa Nchin kupitia filamu yake Royal tour.
Hivi karibun Wakati akizindua safari za treni ya mwendokasi inayotumia umeme SGR Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema safari za treni hiyo itakuwa ni kitovu Cha utalii hapa nchini na watarii watapata fursa ya Kufika mikumi national park Kwa urahisi kabisa.
” ukweli Mhe Rais amekuwa kiongozi hodari na ni Mama mlezi hasa Kwa sisi vijana wake lazima tufanye kazi ili tuweze kumsaidia”
“Alisema kubecha”.