Home Kitaifa MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA MSANGANI MJINI KIBAHA YAPAMBA...

MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA MSANGANI MJINI KIBAHA YAPAMBA MOTO

Zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Msangani Jimbo la Kibaha Mjini unaotarijiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 20 Machi,2024.

Mapema leo Jumamosi Machi 16, 2024 Makarani waongozaji wamepata mafunzo pamoja na kuapa kiapo cha kutunza siri chini ya kanuni ya 16(1) (a) na 50 (4) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 na kanuni ya 14 (1)(a),(2) na 43(4) ya kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa (Uchaguzi wa Madiwani), 2020 mbele ya msimamizi wa Uchaguzi Salum Papen.

Mafunzo hayo yametolewa na Maria Israel na Benjamin Mputtu wakisaidiana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Optuna Kasanda ambao wamewasisitiza kwenda kufanyakazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi

Akifungua mafunzo hayo, msimamizi wa uchaguzi, mwanasheria wa Mahakama Kuu na zilizo chini yake Salum Papen amesema..” Tume imewateua ninyi kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia uzoefu wenu katika masuala ya Uchaguzi katendeni haki” amesisitiza Papen

Papen ametoa rai kwa makarani waongozaji kujiamini na kujitambua, kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi, sheria za uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi na maelekezo mbambali yanayotolewa na Tume

Katika hatua nyingine makarani wametia tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa na chama cha siasa chini ya kanuni ya 16 (1)(b) na ( 3 ) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na kanuni 14(1) (b) na (3) ya kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, (Uchaguzi wa Madiwani), 2020 mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi, Mwanasheria Salum Papen

Aidha, Andrea Isamaki Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ameshiriki kushuhudia mafunzo na kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama kwa makarani waongozaji.

Nadia Issa na Benson Shawa, Makarani waongozaji wamesema wanakwenda kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia S
Sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi

Uchaguzi mdogo Kata ya Msangani unafanyika kutokana na kifo cha Mhe. Leonard Mlowe kilichotokea tarehe 23 Disemba,2023 ambapo jumla ya vyama nane (8) vya Siasa vinatarajia kushiriki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!