Home Kitaifa MAANDALIZI MAONYESHO SABASABA YA 47 YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 98

MAANDALIZI MAONYESHO SABASABA YA 47 YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 98

Na Magrethy Katengu

Maandalizi ya Maonesho ya Sabasaba yanayotarajiwa kuanza Juni 28 mwaka huu yamekamilika kwa asilimia 98 hivyo Wananchi na Wadau wanakaribishwa kushiriki kwani mwaka huu utakuwa wa kipekee .

Akizungumza Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda wakati kifungua Mafunzo ya Wadau wanaotarajiwa kushiriki katika Maonyesho hayo na kufanya ziara ya kutembelea Mabanda yaliyokamilika kutengenezwa amewahakikishia Wananchi kutakuwa na usalama wa kutosha kwani wamejipanga vizuri hivyo wasiewe na wasi wasi Wilaya ya Temeke Iko vizuri

Sanjari na hayo amesema kuwa usafiri upon wa kutosha kwani Mabasi yaendayo haraka yataanzia kubeba abiria kuanzia Gerezani na kuwaleta katika maonyesho kwa bei elekezi kwani hata harabara zake ambazo zinaendelea kujengwa zimekamilika bado kidogo tu na zitatumika katika kipindi hiki cha sabasaba lengo ni kuondoa adha ya usafiri

Niwaase wale wote wanaotumia vyombo vya moto kwakua Sheria ipo ya kuzuia kupita kiholela katika Barbara maalumu zilizojengwa kwa ajili ya kupita Mabasi yaendayo haraka tafadhari ni marufuku kuzitumia barabara hizo tumieni Barbara zenu kwani yeyote atakayekamatwa hatua kali itachukuliwa dhidi yake” amesema Mkuu wa Wilaya

Hata hivyo Munkunda amesema wadau waliomba muda wa maomyesho uongezwe masaa hivyo Mamlaka ya Tantrade wamelichukua wazo hilo na watakwenda kujadiliana na kufanyia kazi .

Aidha Miundo mbinu ya Sabasaba Barbara zimejengwa kwa kiwango cha lami kurahisishia watembea kwa miguu na magari yanayoingia na kutoka kusiwe na vumbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!