Home Kitaifa MAAFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE WAKUTWA NA HATIA YA...

MAAFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE WAKUTWA NA HATIA YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA ILI WATOE AJIRA

Tarehe 30/04/2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Katoki Mwakitalu, imetolea hukumu kupitia Shauri la Jinai Nambari 118 la Mwaka 2023.

Shauri hili ni la Jamhuri dhidi ya;
A) SAMWEL EDSON NGAYAMBA na
B) PAUL IBOJA RICHARD wote Maafisa Utumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

Katika kosa la kwanza, Washitakiwa hawa wakiwa ni Maafisa Utumishi katika Halmashauri hiyo, walishawishi kupewa rushwa ya sh. 1,500,000/= kutoka lwa SIKITU AHMAD NGUGUMO, kama kishawishi ili kumsaidia aweze kupata ajira ya Katibu Mahsusi – Kinyume na Kifungu cha 15(1) na (2) ya PCCA CAP. 329 R.E 2022.

Aidha, katika shtaka la pili, washtakiwa SAMWEL na PAUL walishawishi kupewa rushwa ya sh 1,500,000/= kutoka Kwa BERTHA JOSEPH KIMANUKA kama kishawishi ili waweze kumsaidia kupata ajira ya Katibu Mahsusi, kinyume na Kifungu cha 15(1) na (2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2022.

Pia, katika kosa la tatu, washtakiwa hawa walishawishi kupewa rushwa ya sh 1,500,000/= kutoka kwa ROSE BRYTON KOLANYA kama kishawishi ili waweze kumsaidia aweze kupata ajira ya Katibu Mahsusi, kinyume na Kifungu cha 15(1) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Kosa la nne, Mshtakiwa SAMWEL EDSON NGAYAMBA, akiwa ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kama Afisa Utumishi, alijipatia manufaa kwa njia ya Rushwa, kiasi cha sh. 104,500/= kutoka kwa JOSEPH KIMANUKA MTIAGA ili aweze kumpatia ajira mwanaye aitwaye BERTHA JOSEPH KIMANUKA kwa nafasi ya Katibu Mahsusi, kinyume na Kifungu cha 15(1) na (2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Katika Hukumu, shtaka la kwanza, la pili na la tatu, washtakiwa SAMWEL EDSON NGAYAMBA na PAUL IBOJA RICHARD wametiwa hatiani na kutakiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000/= kwa Kila kosa au kwenda Jela miaka mitatu (3).

Aidha, katika shtaka la nne ambalo linamhusu Mshtakiwa SAMWEL EDSON NGAYAMBA pekee, ametiwa hatiani na kutakiwa kulipa faini ya sh 500,000/= au kwenda Jela miaka mitatu (3).

Washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!