Home Kitaifa MAAFISA USAFIRISHAJI WAHAMASISHA VIJANA KUBORESHA DAFTARI LA MPIGA KURA

MAAFISA USAFIRISHAJI WAHAMASISHA VIJANA KUBORESHA DAFTARI LA MPIGA KURA

Na Mariam Muhando.

MAAFISA Usafirishaji wa Bajaji na Bodaboda Kata ya Upanga Jijini Dar es salaam wameandaa Bonanza la Mchezo wa Mpira wa miguu, ili kuhamasisha vijana kushiriki zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura, linaloanza Jumatau Machi 17,2025, mkoani humo

Akizungumza na City Fm Radio Katika Viwanja vya Shule ya Msingi Upanga Jijini humo Mkurugenzi wa Kik Football Foundation Upanga Magharibi Khalil Karim amesema ameridhishwa na hamasa ya vijana hao

Ninampongeza Muheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwa kinara katika masuala ya michezo hivyo tunamuombea Rais wetu katika Uchaguzi Mkuu, aweze kupata miaka mitano mingine ya kuliongoza Taifa letu”,Alisema Karim

Nao Baadhi ya Maafisa hao wamempongeza Kiongozi huyo Kwa kuwaunga mkono katika masuala ya michezo kwani ni Moja ya chachu katika kuhamasha Vijana kujitokeza kwenye zoezi hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!