Kuelekea wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Mwaka huu kitaifa yanatarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza huku ikiwa na kauli mbiu inayosema; Tanzania bila ajali inawezeka timiza wajibu wako na ikitarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 hadi 17 Mwezi Machi Mwaka huu Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mhe. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Ramadhan Ng’anzi, amesema kuanzia February Mosi, 2023 magari yote ya Mkoa wa Mwanza yataanza kukaguliwa katika vituo vitakavyoteuliwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa huo Sunday Ibrahimu “Natoa wito kwa watumiaji wote wa vyombo vya moto nchi nzima waanze kukaguliwa mapema kabla ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani , baada ya wiki hiyo gari itakayokamatwa ikiwa haijakaguliwa itachukuliwa hatua kali za kisheria. ” Tumejipanga kikamilifu kuyakagua magari na vyombo vyote vya moto nchi nzima baada ya ukaguzi watapewa cheti maalum yaani stika ya ukaguzi,” Amesema Ng’anzi
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Adam Malima ” Magari makubwa ya mizigo yanayotaka kuingia mjini yafike kuanzia saa tano usiku hadi saa 11 alfajiri lengo ni kuepusha msongamano wa magari unaoweza kusababisha ajali, yakifika mapema yapaki stendi ya Mabasi Nyamhongolo kuna maeneo makubwa yametengwa kwa ajili ya magari makubwa
Aidha Malima amewataka madereva wote wa magari makubwa endapo magari yao yataharibika yaiwa barabarani wahakikishe wanayatoa barabarani ndani ya saa mbili tangu liharibike ukipita muda huo vyombo vya ulinzi na usalama watalitoa kwa gharama za mwenye gari
“Wenye magari na madereva nawashauri watakapokuwa wanakuja mkoani Mwanza kama magari yao ni mabovu wasiyaingize ndani ya mkoa huu maana likiharibika likiwa barabarani litaondolewa na watafidia gharama za kuliondoa barabarani,Malima
“Unakuwaje na gari lenye thamani ya Sh milioni 100 halafu unashindwa kutengeneza tatizo la Sh milioni tatu huo ni uzembe hivyo ukiingiza gari bovu barabarani likaharibika utalitoa kwa ghara zako na tukilitoa sisi utalipa pamoja ma fidia,” Malima
“Hii tabia ya kuacha magari kwenye maeneo hatarishi unakuta limeharibika kwenye kona kali limekaa barabarani siku tatu wanaweka majani mkoa wa Mwanza tumepiga marufuku maana inasababisha ajali inayoweza kuepukika,” Malima
“Mkoa wa Mwanza tumekubali kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa mwaka huu 2023 yatakayofanyika katika uwanja wa Furahisha, hatutaadhimisha kwa kuweka mahema bali kwa kuhakikisha watu wote wanaotumia barabara wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,” Malima. Mwisho